Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Rosemary Senyamule amewapa siku 30 wananchi wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha katika vituo vya Polisi kwa usalama wao kwani baada ya muda huo hataki kulaumiwa kwa lolote litakalo fanyika.

Na katika kufanikisha suala hilo ameagiza jeshi la Polisi kuwachunguza askari wake wenye tabia ya kuwa na urafiki na watu wanao tuhumiwa katika makosa mbalimbali huku akisisitiza kutowaacha salama na kuwashughulikia kwa mujibu wa maadili ya utumishi.

” Kuna kesi kwamba kuna askari baadhi wana urafiki na watu wanaotajwa kuhusika katika makosa mbalimbali sasa kitendo hicho kinakwamisha jitihada za kudhibiti uhalifu wilayani kwangu, ninachokiona ni kuanza na hao kwanza kisha waje wahalifu wenyewe” amesema Senyamule.

Senyamule ametoa agizo hilo kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama iliyokutana kwaajili ya kujadili pamoja masuala ya hali ya usalama wilayani humo ambapo watu watano wanye silaha walikamatwa.

Ameeleza kuwa kukamatwa kwa watu hao na silaha kunaonyesha uwepo wa watu wenye silaha majumbani kinyume na sheria jambo ambalo anaona halikubaliki kwenye wilaya yake.

Aidha amebainisha kuwa Serikali ya wilaya hiyo inajipanga kwaajili ya watakaokaidi agizo hilo kwa kuanzisha msako wa nyumba hadi nyumba, shamba hadi shamba na shimo hadi shimo na kuhakikisha hakuna silaha inayomilikiwa kinyume na sheria.

AT ampiga 'stop' mkewe kupika "alishawahi kuwekewa sumu"
Mwandishi aliyetekwa miaka mitatu Syria aachiwa huru