Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Robert Boaz, ametoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao ya jamii kwa lengo la upotoshaji na kuliagiza Jeshi la polisi kuanza mara moja kuwashughuliakia na kuwachukulia hatua za kisheria watu wenye tabia hiyo.

Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi huyo mara baada ya mitandao ya kijamii kusambaza video yenye habari inayonyesha uwepo wa mchele wa plastiki nchini.

Boaz amekanusha uwepo wa mchele huo wa plastiki na kumsaka kwa udi na uvumba mtu aliyerekodi video hiyo ili asaidie kutoa taarifa zaidi.

Na amewaomba wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kujiepusha kusambaza taarifa zisizokuwa na ukweli, kwani ni hatari na husababisha madhara makubwa katika jamii.

”Kabla ya kusambaza taarifa kwanza uwe na uhakika wa vyanzo vyako, wahsuika wanaweza kuingia kwenye matatizo yasiyokuwa ya msingi”. amesema Boaz.

Aidha waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia na wazee na watoto , Ummy Mwalimu ametaarifiwa na  Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), kuwa hakuna mchele wa aina hiyo nchini.

Waziri Ummy amewasisitizia watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, na kuepuka upotoshaji.

Video: Majaliwa akabidhi pikipiki 49 kwa vijana Ruangwa
Kenya wamtaka mchungaji kumfufua Nkaissery