Kiungo mshambuliaji wa Man City , Kevin De Bruyne  amefunguka na kusema asingeihama Chelsea ingemlipa vizuri.

Staa huyo raia wa Ubelgiji alisema anaamini angekuwa na mchango mkubwa Stanford Bridge, lakini alikuwa akilipwa mshahara mbuzi ndio maana akaamua kutimka.

Aliongeza kusema kuwa pia kocha wa City, Manuel Pellegrini amemuamini sana na kumpa nafasi tofauti na ilivyokuwa kwa Jose Mourinho.

Kevin De Bruyne alitua Chelsea akitokea Genk ya Ubelgiji Januari mwaka 2012 kwa ada ya paundi mil. 7 lakini akaondoka mwaka 2014 kwenda Wolfsburg ya Ujerumani.

Kile alichokionyesha katika Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ kilikuwa tofauti na mtazamo wa wengi, aling’aa na kuzifanya timu nyingi kumbabaikia lakini City ni waliomtwaa kwa fedha ndefu na ahadi ya mshahara mnono.

Kwa sasa ndani ya City, De Bruyne anachukua mshahara kwa wiki baada ya klabu hiyo kukubali kulipa paundi mil. 55 kuinasa saini yake, laini tayari amekuwa mmoja wa wachezaji muhimili wa timu licha ya umri wake mdogo wa miaka 24.

Pellegrini Aendelea Kujitisha Kwa Kivuli Chake Man City
Kawemba: Tuna Uchu Na Ubingwa Wa Mapinduzi