Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Kevin De Bruyne amemkingia kifua beki wa pembeni kutoka England na klabu ya Manchester City Kyle Walker, baada ya mchambuzi wa soka Roy Keane kumsema vibaya kutokana na kiwango chake alichoonesha mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool ambao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Katika mchezo huo Walker alisababisha mkwaju wa Penati uliopigwa na Mohamed Salah na kuifanya Liverpool kuongoza kwa muda wa dakika 13, kabla ya Manchester City kusawazisha kupitia kwa Gabriel Jesus dakika ya 31.

De Bruyne ambaye pia ni mchezaji wa klabu ya Manchester United amesema Walker ni mchezjai wa kpekee na wa tofauti sana kwenye kikosi chao, hivyo haikuwa jambo jema kutupiwa lawama.

“Ni miongoni mwa wachezaji ambao ni wagumu sana kukumbana na majeraha, ni tegemeo na anajua nini maana halisi ya kukaba,”alisema.

“Huwezi kumfananisha Kyle na Trent Alexander-Arnold wa Liverpool kwa sababu ni wachezaji wawili tofauti, Trent ni mchezaji anayeweza zaidi kushambulia na Kyle huwa anaweza kucheza kwa kushambulia  na kuzuia,”aliongeza.

Keane ni miongoni mwa wachambuzi wachache waliosema hadharani kuhusiana na mchezaji huyo ambaye akisema Walker huwa hajifunzi licha ya kucheza soka kwa muda mrefu lakini De Bruyne alisema Walker hajaliweka suala hilo katika kichwa chake na ni jambo la kawaida upande wake.

“Roy Keane ni mtu wa tofauti sana na kila mtu anafahamu hilo, lakini huo ni mtazamo wake  na naamini Walker atakuwa sawa baada ya mapito haya na hajachukulia kauli hiyo kama sehemu ya lawama bali ni sehemu ya changamoto.”

Walker alijiunga Manchester City Julai, 2017 kwa dau la Euro 52 milioni mpaka sasa amechukuwa mataji mawili ya EPL.

Msimu huu amecheza michezo 12 katika michuano yote na kufunga bao moja.

Mwili wa askari aliyedaiwa kuuawa Pemba wapatikana
Tshala Muana mikononi mwa Polisi