Baada ya harakati za kutaka kuihama Man Utd na kujiunga na klabu ya Real Madrid katika usajili wa majira ya kiangazi kukwama, mlinda mlango kutoka nchini Hispania David de Gea Quintana, amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 kitakachopambana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2015-16.

De Gea alikua aliachwa pembeni ya kikosi cha Man utd ambacho kilikua na mtihani wa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo, dhidi ya Club Brugge ya nchini Ubelgiji, kwa kusudio la kuangalia uwezekano kama angeweza kutimiza ndoto zake za kurejea nyumbani Hispania.

Kujumuishwa kwenye kikosi hicho, kunaamisha mambo yamekaa sawa sawa kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 24, na sasa huenda akawa sehemu ya wachezaji ambao watarejeshwa kwenye kikosi cha kwanza kufuatia uwezo mkubwa alionao.

Hata hivyo katika orodha hiyo iliyowasilishwa UEFA, jina la aliyekua mlinda mlango wa FC Barcelona, Víctor Valdés Arribas limeachwa, hivyo hatoweza kucheza michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya klabu.

Valdes amekua na mkwaruzano na meneja wa klabu ya Man Utd, Louis Van Gaal tangu mwezi July wakati kikosi cha mashetani wekundu kilipokua kikijiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi unaoendelea.

Kwa sasa De Gea amerejea nyumbani Hispania kuitikia wito wa timu ya taifa lake, ambayo itakua na mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya dhidi ya Slovakia pamoja na Macedonia.

Katika orodha ya Man utd iliyowasilishwa UEFA, tayari kwa kupambana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, wapo wachezaji wote waliosajili katika kipindi cha majira ya kiangazi kama Anthony Martial aliyesajiliwa siku ya mwisho ya dirisha la usajili akitokea AS Monaco kwa ada ya paund million 36, mlinda mlango Sergio Romero, Matteo Darmian, Bastian Schweinsteiger, Morgan Schneiderlin pamoja na Memphis Depay.

Kikosi cha Man Utd kitakachopambana na kuhakikisha kinajitetea kwenye mipango ya kutwaa ubingwa wa barani Ulaya msimu wa 2015-16, upande wa makipa yupo David De Gea, Sergio Romero, Sam Johnstone

Mabeki: Phil Jones, Marcos Rojo, Chris Smalling, Luke Shaw, Guillermo Varela, na Paddy McNair.

Viungo: Michael Carrick, Daley Blind, Ashley Young, Ander Herrera, Nick Powell, Antonio Valencia, Marouane Fellaini, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, Jesse Lingard, Andreas Pereira na Juan Mata

Washambuliaji: Memphis Depay, Anthony Martial, Wayne Rooney na James Wilson

Mkwasa Afurwhishwa Na Ukamilifu Wa Kikosi
Pacquiao Kuachana Na Masumbwi 2016