Mshambuliaji kutoka nchini Serbia wa Simba SC Dejan Georgijevic ameushtua umma wa Mashabiki wa Soka nchini Tanzania kufuatia ujumbe aliouandika katika Ukurasa wake wa Instagram muda mchache uliopita.

Dejan aliyesajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya Nogometni klub Domžale inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Slovenia, ameweka ujumbe unaothibitisha kuvunjwa kwa mkataba wake na klabu hiyo ya Msimbazi.

Mshambuliaji huyo ambaye aliambatana na kikosi cha Simba SC hadi Kisiwani Unguja-Zanzibar kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Malindi na Kipanga FC ameandika: “Ninathibitisha kwamba Mkataba wangu wa ajira umesitishwa kwa sababu za haki kutokana na ukiukwaji wa kimsingi wa Mkataba na Klabu.”

“Asanteni mashabiki kwa ushirikiano na upendo mlionipa.”

Mara ya mwisho Dejan alionekana akiwa na kwenye kikosi cha Simba SC katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Malindi FC, uliomalizika kwa wenyeji kukubali kichapo cha 1-0.

Dejan anaondoka Simba SC akiwa ameifungia bao moja, huku akikosa nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo katika michezo ya Kimashindano tangu aliposajiliwa mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Waandamana kulipongeza Jeshi la Polisi
Singida Big Stars yaiwahi Azam FC Dar es salaam