Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Deo Kanda amesema ikitokea Uongozi wa Simba SC unahitaji huduma yake kwa msimu ujao, hatokua na hiyana ya kurudi klabuni hapo, kutokana na kutambua umuhimu wa kazi yake.

Kanda aliondoka Simba SC mwishoni mwa msimu wa 2019/20, baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo akitokea TP Mazembe, ambayo ilihitaji kumuuza jumla kwa kiasi kikubwa cha pesa, ambacho kilipingwa na Viongozi wa Msimbazi.

Kanda ambaye kwa sasa yupo Mtibwa Sugar na huenda leo Alhamis akacheza mchezo wa Mzunguuko wa 28 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC, amesema kazi yake ni kucheza soka, anaamini ana uwezo wa kucheza katika kiwango cha hali ya juu, hivyo yupo tayari kucheza tena Msimbazi.

“Kama itatokea viongozi wa Simba SC wananihitaji nipo tayari kurudi, unajua kazi yangu ni kucheza soka, kwa hiyo ikitokea hiyo nafasi nitakwenda na ninauhakika nitacheza”

“Kwa sasa nipo Mtibwa Sugar, lakini soka linaweza kukuhamisha wakati wowote, kama Simba SC watakua tayari watazungumza na viongozi wa hapa na nitaondoka, lakini nisisitize kwamba ninaheshimu sana mkataba wangu na Mtibwa Sugar.” Amesema Kanda

Deo Kanda alisajiliwa Mtibwa Sugar wakati wa Dirisha Dogo la Usajili mwishoni mwa mwaka 2021, lakini alikua na changamoto ya kukosa Kibali Cha Uhamisho wa Kimataifa ‘ITC’ kutoka TP Mazembe.

Mwanzoni mwa mwezi huu Mchezaji huyo alifanikiwa kupata ITC yake, sasa yupo huru kucheza soka akiwa na klabu yake mpya wa Mtibwa Sugar, leo huenda akawa sehemu ya kikosi kitakachoivaa Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mauzo medali ya dhahabu kusaidia watoto wakimbizi
Tetemeko laua watu zaidi ya 1,500