Dereva wa lori aina ya HOWO anadaiwa kuiba pipa 156 ya lami yenye thamani ya zaidi ya Sh35 milioni na kusambaza maeneo mbalimbali wakati akiwa njiani kusafirisha kwenda kwa mteja mkoani Arusha.

Dereva huyo anadaiwa kuiba mali hiyo ya kampuni ya biashara na usafirishaji  Tanzania (CRSG) Kibaha, wakati akiwa njiani kuelekea Arusha ambapo alifungua king’amuzi (GPS) kwenye gari hilo na kisha kushusha pipa idadi tofauti tofauti kwenye maeneo tofauti kisha kulitelekeza.

Akithibitisha kutokea kwa wizi huo, Kamanda wa Polisi Pwani, Wankyo Nyigesa amesema kuwa taarifa za upotevu wa pipa hizo ilitolewa na ofisa usafirishaji wa CRSG, Zediel Mendes ambapo ufuatiliaji na upelelezi ulianza na kubaini kuwa dereva huyo alipita mzani ya Msata Chalinze lakini alipofika Segerea Tanga alitoa GPS kwenye gari na kugeuza hadi eneo la Kabuku na kushusha pipa 134.

“Huyu dereva alianza safari vizuri maana ameonekana alipita mizani yote, lakini gari ikiwa safarini maeneo la Segera Tanga alinyofoa king’amuzi GPS ya kwenye hilo lori hivyo maafisa wa kampuni wakawa hawaioni tena, walipotia shaka walitoa taarifa na kufaniwa kubaini huu mchezo uliofanyika na tayari tumepata pipa 72 na watuhumiwa tisa” amesema Nyigesa.

Amesema kuwa uchunguzi huo wa awali umebaini pia dereva huyo alirudi na pipa 22 na alipita mizani ya Msata tena ila alipofika Chalinze alishusha hayo yaliyobakia na kuendelea na safari kuelekea iliko kampuni hiyo ambapo akiwa eneo la Mkuza Kibaha aliitelekeza lori hilo kisha kutoweka.

Akibainisha tukio hilo ofisa usafirishaji wa CRSG, Mendes amesema kuwa kampuni hiyo katika kuhakikisha usalama wa mali na wafanyakazi hasa madereva magari yao yote wamefunga GPS na njia hiyo ndio iliowezesha kutambua mapema kuwa gari moja limepata shida na katika kufatilia ndio wakabaini ilifunguliwa king’amuzi icho kwa lengo la kuipoteza kwenye ramani ili uhalifu huo ufanyike pasiposhaka.

“Dereva huyo kwa kudhani akifungua GPS atafikia malengo yake amejikuta akinaswa kilaini na baadhi ya pipa zetu tumeanza kuzipata na tunaishukuru Polisi kwa kweli wametoa ushirikiano maana pipa 22 tulikamata Chalinze na  50 huko nane nane Morogoro yakiwa yalishaanza kusambazwa kwenda kuuzwa” amesema Mendes.

Ramaphosa aifagilia Ujerumani
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 22, 2018

Comments

comments