Dereva wa gari la mafuta lililopata ajali mkoani Ruvuma na kuhofiwa kufariki dunia amepatikana akiwa hai katika hospitali ya mkoa Manispaa ya Songea.

Dereva huyo hakuonekana baada ya kutokea kwa ajali hiyo, ambapo kichwa cha gari kiliteketea chote kwa moto. ambapo baada ya kupatikana alikutwa na michubuko pamoja na mbavu kuvunjika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa amesema uchunguzi zaidi unaendelea kujua chanzo cha ajali hiyo, ingawa shehena ya mafuta yote aliyokuwa amebeba imekutwa salama.

Gari aina ya Scania yenye namba za usajili T243DTV, ikiwa na mafuta ya petroli lita 33,000, mali ya James Mwinuka ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Njombe Filling Station, ilipata ajali usiku wa Jumapili ya Agosti 11 ,2019 ambapo tenki la mafuta hayo lilibaki bila kuteketea kwa moto.

Aidha, kamanda Marwa amelitaja jina la dereva aliyepata ajali hiyo kuwa ni Hubert Mtete, aliyekuwa akitokea Njombe kuelekea Songea.

Mabalozi 42 kutembelea mradi wa JNHPP uliopo Rufiji
Tanzania yapokea Uenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri SADC