Matarajio ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kujua hatma ya kesi yake leo yameyeyuka baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kushindwa kutoa uamuzi kuhusu rufaa ya upande wa Jamhuri kupinga dhamana ya mwanasiasa huyo.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma Maghimbi alisema kuwa hawezi kuendelea na maamuzi kuhusu dhamana ya kesi hiyo kwani upande wa Jamhuri umewasilisha notisi ya kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa.

Lema alipewa dhamana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha mwezi Novemba mwaka jana lakini upande wa Jamhuri ulizuia kwa kuwasilisha notisi ya mdomo kuhusu hatua waliyoichukua ya kukata rufaa katika Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo wa kutoa dhamana.

Katika kesi ya msingi, Lema anashtakiwa kwa kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Kambi ya Rais Mteule wa Gambia yanena kuhusu taarifa za kupigwa risasi
Sheria kuhusu wanawake wawapo kwenye hedhi yazua gumzo Zambia