Mshambuliaji wa pembeni kutoka Argentina, Angel Di Maria yuko njiani kusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kuendelea kuitumikia klabu bingwa nchini Ufaransa, Paris Saint-Gemain.

Taarifa kutoka jijini Paris zinaeleza kuwa, mshambuliaji huyo atasaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamuwezesha kuwepo jijini hapo hadi mwaka 2021.

Akiwa katika mkutano na waandishi wa habari ulipokua unazungumzia mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo PSG watapambana na FK Crvena Zvezda, mshambuliaji huyo aliulizwa kuhusu mustakabali wake.

Di Maria alisema mustakabali wake ndani ya PSG upo vizuri na angependa kuendelea kuwepo klabuni hapo kwa miaka mingine zaidi, kutokana na kupendezwa na mazingira ya klabu hiyo.

“Siku zote nimekua na furaha ya kuendelea kuwa mchezaji wa PSG, mazingira ya kucheza soka langu nikiwa hapa ninayafurahia sana,” alisema.

“Tusubiri na kuona nini kitatokea katika suala la mkataba wangu mpya, lakini ninafurahia kuwa sehemu ya kikosi cha PSG, kila mmoja miongoni mwetu analifahamu hilo.”

Di Maria amekua mchezaji anaefurahia mfumo wa meneja mpya wa klabu ya PSG Thomas Tuchel, na amekua mchezaji ambaye ameshacheza katika kikosi cha kwanza mara zote tangu msimu huu ulipoanza.

McGregor aahidi kumpasua Khabib Jumamosi hii
Video: Zitto, Serikali kuliamsha tena, Janga jipya lanyemelea wafiwa wa MV Nyerere

Comments

comments