Mwimbaji Diamond Platinumz ambaye siku zote amekuwa akisema humchukulia rapa Chidi Benz kama kaka yake, amefanya kile kilichofanywa na rapa huyo miaka kadhaa iliyopita na kukosolewa na wengi.

Moja kati ya watu waliowahi kuikosoa wazi hatua hiyo ya Chidi Benz ni rapa Nay wa Mitego ambaye ni swahiba wa Diamond Platinumz.

Diamond ameamua kuweka ‘kipini’ kwenye pua yake (japo haijafahamika kama ametoboa au amebandika tu). Picha za hivi karibuni zimemuonesha muimbaji huyo aliyeenda mapumzikoni na familia yake jijini Paris Ufaransa, akiwa katika muonekano huo mpya.

?

A photo posted by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Muonekano huo umepokelewa kwa mtazamo tofauti na mashabiki wake pamoja na kambi hasimu ya ‘Team Diamond Platinumz’. Diamond na Kipini Hata hivyo, baada ya muda alipost picha nyingine ikimuonesha akiwa hana kipini puani na isiyoonesha tundu puani kwake.

Mapenzi: Faida ya Kuvaa socks miguuni wakati wa tendo la ndoa
Makala: Kagame alivyozika 'tofauti' na JK na kufufua Urafiki mzito na JPM (Picha)