Baada ya kuichafua mitandao na video zake zilizowaacha midomo wazi wale wa kizazi kipya huku wahenga ‘wakitema mate chini’, Diamond Platinumz arejea kivingine.

Mkali huyo ambaye hivi sasa anaitangaza kwa nguvu zote ngoma mpya aliyofanya na Harmonize, ‘Kwangwaru’, ambayo nayo pia BASATA wanaiangalia kwa darubini kali, amefuta kichwani matukio hayo ya juzi kwa kuweka picha zinazomuonesha akiwa kwenye mkuta wa kibiashara na makampuni makubwa mawili nchini, kwa nyakati tofauti.

Akiwa na yuleyule Harmonize ambaye saa chache kabla alionekana kwenye video zile akiruka ‘sarakasi’ wakati Bosi wake huyo akiwa anacheza na mwili wa mrembo mwenye asili ya bara Asia pamoja na mzazi mwenzake Amisa Mobeto, Baba Tifah alizungumza kibiashara na Bank ya Afrika (BOA) akiwa ndani ya suti ya matawi ya juu aliyoyaimba Langa.

“Superb Meeting with BOA bank… what a great Monday… Na kasuti kangu hapo kama sio mie wa Jana Vile… Work Hard and Play Harder,” aliandika kwenye picha mbili alizoambatanisha.

Katika picha nyingine, Diamond amekutana na uongozi wa Star Times kuhakikisha Wasafi TV inapatikana kwenye king’amuzi hicho kinachotumiwa na watu wengi zaidi nchini.

Ni Diamond yuleyule, wa jana na juzi na wa leo, hatabiriki lakini kuna jambo! Endelea kuifuatilia Dar24…

Mkuchika awatahadharisha viongozi wanao wabania Walimu
Serikali kumwaga ajira 49,356 mwaka wa fedha 2018/19

Comments

comments