Mwanamuziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz ambaye pia ni Balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, amekabidhi kompyuta kwaajili ya masomo kwa watoto yatima kwenye kituo cha Huruma Islamic na Amani Foundation.

Ametoa msaada huo ili kuwawezesha watoto kujifunza na kuendana na kasi ya teknolojia, kujiandaa vyema na mahitaji ya soko la ajira duniani. Pia Diamond amekabidhi runinga, jenereta na vyakula kwa vituo hivyo viwili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Diamond Platnumz amesema kuwa anapenda kufanya kazi na kampuni zinazothamini watu kwenye jamii, sio kuangalia biashara tu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana amesema kwamba wanapenda umma utambue kuwa kampuni yao imejengwa katika misingi ya kusaidia jamii hususani katika nyanja za elimu, michezo, na mazingira.., Bofya hapa kutazama

DOREFA kusaidia usajili Dodoma FC
Wachina 2 mbaroni kwa kudukua chanjo ya Corona Marekani