Diamond Platnumz amempongeza Ali Kiba kwa uamuzi wake wa kufunga pingu za maisha na mrembo kutoka Mombasa, Aminah. Tukio hilo lilioneshwa kupitia kituo cha runinga cha Azam.

Bosi huyo wa WCB ametumia mtandao wa Instagram kumtakia heri Mfalme Kiba wa Bongo Fleva kwa hatua aliyoipiga akivuka maisha ya ujana.

“Ni Mwendo wa Picha za Suti tu sasa hivi, Maana nisije nikafungua hata kashati nikajikuta Centro…Pole yenu Wa zee wa Gym, Kama Muscat Round hii???…. Wadau Nimeambiwa King Kiba kaoa leo…Mfikishieni Salam zangu, za Ndoa njema, na Maisha yenye Furaha, Amani na Baraka tele…??? #SanaaImezaliwaUpya #KWANGWARU

Maandishi ya Diamond na picha aliyoiweka akiwa na Harmonize yalimuamsha dada yake, Esma aliyemtaka naye aige mfano wa Ali Kiba.


Mama yake Diamond pia amepost picha ya Ali Kiba akiwa na mkewe Aminah na kuwapa hongera na kuwaombea heri ya maisha ya ndoa.

“Bismillaah mashallah Hongera sana @officialalikiba kwa kupata Mke, nawatakia maisha mema yenye mafanikio na furaha tele kwenye ndoa yenu, Mungu awabariki sana,” ameandika Mama Diamond, akiweka picha ya King Kiba na Malkia wake.

 

Swaziland sasa kuitwa eSwatin
Video: Zitto rudi darasani, hujui hesabu- Polepole