Bosi wa lebo ya WCB, Diamond Platinumz amemuomba Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kusitisha mpango wake wa kumzungumzia kesho kanisani kwake kwa lengo la kumuadhibu.

Diamond amechukua uamuzi huo muda mfupi baada ya Askofu Gwajima kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akieleza kuwa ataiegeuza almasi (diamond) kuwa maji kutokana na kughafirishwa na jinsi alivyotajwa kwenye wimbo mpya wa msanii huyo ‘Bora Nikae Kimya’.

“Aliyeniweka kwenye wimbo kwa lengo la kupotosha HAKI ili kusapoti vyetu feki, Jiandae ALMASI ITAGEUKA MAJI kesho!” aliandika Gwajima kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Muda mfupi baadae Diamond alitumia mtandao huo kutoa ufafanuzi wa kile alichokiimba huku akimsihi Askofu huyo kuahirisha mpango wake. Mondi alitoa ufafanuzi wa namna na sababu za kuwataja  Gwajima, ‘Konda’ [Inayosadikika kuwa ni ufupisho wa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa WCB na binti mmoja mtandaoni.

Roma Azungumza Kwa Mara ya kwanza Baada ya 'Kupatikana'
DC Mjema apiga marufuku shughuli za uchimbaji kokoto eneo la Pugu