Nasibu Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz, amepagawaisha mashabki kwenye tamasha la nne la sanaa na utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) lilofanyika uwanja wa uhuru jijini Dares Salaam.

Tamasha hilo lililozinduliwa na makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan huku watu mbalimbali kutoka Afrika Mashariki walijitokeza kwa wingi jana kwenye tamasha hilo.

Msanii huyo alitumbuiza dakika chache kabla ya kusimamishwa na kisha msanii huyo kwenda kumsalimia mgeni rasmi, na baadae diamond aliendelea na burudani ambayo aliisimamisha zaidi ya dakika 30.

Nyimbo za msanii huyo ambazo tayari zimeshatikisa majukwaa mbalimbali ikiwemo, kanyaga ,Tetema, Number One , kitolondo, na zingine nyingi ndizo ziligusa sana mashabiki wake.

Shoo hiyo ilikuwa ya aina yake huku madansa wa Diamond zaidi ya 20 wakiwa wamevaa nguo nyeusi  na viatu vyeusi wakati huo msanii mwenywe ambaye mashabiki walikuwa wanamuita jina la ‘simba’ alivaa nguo za njano na baadae kuvua na kubaki tumbo wazi ilipelekea aadhi ya mashabiki na wao kuvua fulana zao.

Fatma Karume ageukia siasa
Ndege yaanguka hifadhi ya Serengeti yaua wawili

Comments

comments