Msanii wa bongo fleva ambaye amewahi kufanya kolabo na Diamond, Hawa Mayoka katika kibao chao cha ”Nitarejea” amemshukuru sana Daimond kwa kuamua kumsaidia kumchangia pesa milioni 50 zitakazo msaidia kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa kipindi kirefu Hawa amekuwa akisumbuliwa na tatizo la ini ambalo limekuwa likimsababishia miguu na tumbo kujaa maji mara kwa mara, jitihada za madaktari hapa nchini kumaliza tatizo hilo zimegongwa mwamba na ametakiwa kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.

Hawa amemshukuru sana Diamond kwa kuamua kumsaidia kwani alikuwa ameshakata tamaa ya kupona kutokana na hali duni ya kifedha.

Hawa amesema hajawahi kufikiria kama ipo siku Diamond atamkumbuka na kumsaidia kwa kiasi kikubwa namna hiyo.

”Nilishakata tamaa kabisa ya kupata matibabu kutokana na uwezo wa kifedha kuwa mdogo kwani madaktari wa hapa walisema natakiwa kutibiwa India, kwa sasa nimepata tumaini baada ya Diamond kujitolea kunipeleka kwenye matibabu India amesema Hawa.

Hivi karibuni Diamond aliahidi kumsaidia msanii huyu pesa yenye thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya matibabu nchini India.

Aidha mama wa Hawa ambaye amekuwa akimuuguza amemshukuru sana Diamond kwa kuamua kumsaidia mtoto wake.

”Yaani hapa sijui nianzie wapi ni kumshukuru Mungu tu ambariki Diamond maana naona kabisa anenda kuokoa maisha ya mwanangu” amesema Ndigina Said.

Igor Akinfeev aheshimu wakati
Tha Carter V yaanza kukwea kilele, yaweka rekodi