Bosi wa WCB, Diamond ametoa maoni yake kuhusu agizo la Rais John Magufuli alilolitoa hivi karibuni kuwa hakuna mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari atakayeendelea na masomo baada ya kupata ujauzito.

Akiwa jijini Kigali nchini Rwanda alipoenda kufanya biashara ya muziki wake, Diamond alisema kuwa hawezi kupinga agizo la Rais Magufuli kwani Watanzania wengi walimuamini na kumpa nafasi ya urais.

“He is the president (ni Rais), so siwezi kubisha, mpaka alipochaguliwa kuwa rais, ina maana tumekubaliana na akili yake tumeona anafaa,” alisema Diamond.

Msanii huyo aliongeza kuwa hawezi kujua kwanini Rais Magufuli alitoa uamuzi huo kuhusu wanafunzi wa kike wa shule za sekondari na shule za msingi.

Agizo hilo la Rais Magufuli lilizua mijadala mingi kwa watu wanaoiunga mkono na wale wanaoona ilipaswa kuwa vinginevyo. Mijadala hiyo imevuta usikivu wa vyombo vya kimataifa na nchi jirani.

Tume ya uchaguzi Kenya yajibu kuhusu 'marehemu kupiga kura'
Baba yake Michael Jackson apata ajali ya gari, afya yake yaripotiwa