Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz ametajwa katika vipengele sita katika tuzo za AFRIMA 2021

Waandaaji wa tuzo hizo wametangaza listi ya wasanii wa bongo fleva watao wania tuzo hizo kwenye vipengele mbalimbali.

Kwa upande wa Tanzania, listi hiyo inaongozwa na diamond Platnumz ambaye jina lake limetajwa kwenye vipengele sita.

Wasanii wengine waliotajwa ni Nandy, King Kiba, Harmonize, Darassa, Rosa Ree na Zuchu.

Kwa upande wa ma-DJ, Tanzania inawakilishwa na DJ Sinyorita kutoka Clouds FM huku watayarishaji wa muziki wakiwakilishwa na Lizer Classic na watayarishaji wa video wakiwakilishwa na Director Kenny.

Kwenye listi hiyo msanii anayeongoza ni Kundi la Blaq Diamond kutoka Afrika Kusini ambao wametajwa kwenye vipengele nane.

Namba mbili inashikiliwa na Focalistic ambaye ametajwa kwenye vipengele saba na namba tatu inashikiliwa na Wizkid ambaye ametajwa kwenye vipengele sita.

Video: Wenzetu walichinjwa kama kuku
Biteko:Mirerani haitageuzwa shamba la bibi