Mwezi Agosti ndio mwezi ambao mtoto wa kwanza wa msanii Diamond Platinumz na Zarina Hassan alizaliwa, Tiffah Naseeb kufuatia sherehe hiyo Diamond Platinumz ametangaza ofa ya kuwasafirisha watu 30 mpaka Afrika Kusini kusherekea siku hiyo ya kuzaliwa kwa mwanae ya kutimiza miaka mitatu.

Diamond amesema sherehe hiyo itachukua siku tatu ambayo ni ijumaa, jumamosi na jumapili, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika.

”Kwakuwa sherehe hii ya kutimiza miaka mitatu kwa Binti angu @princess_tiffah itachukua WeekEnd nzima, yani kuanzia Ijumaa/ Jumamosi na Jumapili ….kwenye kuhakikisha watu wangu hao 30 wanasafiri Salama, wanakula na wanalala sehemu nzuri na kuwa comfortable siku zote wakiwa huko” ameandika Diamond Platinumz.

Sherehe hiyo itarushwa mubashara kupitia kituo cha runinga cha Wasafi.

Aidha haijafahamishwa bado namna itakayotumiwa kuwapata watu hao 30 watakaosafiri mpaka Afrika Kusini kusherekea siku ya kuzaliwa kwa Tiffah.

Cristiano Ronaldo kukosa ziara ya Marekani
CSKA Moscow waitaka Chelsea kufuata taratibu

Comments

comments