Msanii mkongwe wa nyimbo za asili, Saida Karoli amefunguka na kuweka wazi kuwa ameambulia patupu kutoka kwa baadhi ya wasanii waliotumia mdundo (beat) wa nyimbo yake.

Saida Kalori amesema kuwa mpaka sasa hajawachukulia hatua na hatafanya hivyo kwani anaamini kuwa hata kama wasanii hao wasingetumia wimbo huo bado kuna wasanii wengine baadaye wangetumia na daima utaendelea kuwa juu.

Amesema kuwa msanii kama Diamond Platinum alifanya nae makubaliano kuwa katika mapato ambayo yangepatikana kutoka kwenye wimbo huo, ambao Diamond Platinum aliuita Salome huku akimshirikisha Rayvany, aliahidi kumpa Saida Karoli asilimia 25 lakini hadi sasa hakuna chochote alicholipwa na msanii huyo.

Saida Karoli alitaja wengine ambao walitumia nyimbo yake ya chambua kama karanga bila makubaliano wala malipo yeyote ni pamoja na msanii Belle 9, katika wimbo wake wa ‘give it to me’ na Msanii Darassa katika wimbo wake wa ‘Muziki’

 

Suma JKT kufungua kiwanda cha kusindika minofu
Vichwa vya treni vyazua utata bandarini, TRL yakana kuvimiliki