Mmiliki wa Lebo ya WCB, Abdul Naseeb ‘Diamond Platinumz’ ameonekana kuwa na utayari wa kuiwasha upya nyota ya mkali wa zamani wa miondoko ya Takeu, Lucas Mkenda maarufu kama Mr. Nice ambaye nyota yake ilizimika ghafla baada ya kutamba na kufanya vizuri katika muziki miaka ya nyuma.

Hayo yamedhihirishwa mara baada ya mmoja wa msanii anayesimamiwa na Diamond Platinumz chini ya lebo ya WCB, kutoa kichupa chake kipya kinachoenda kwa jina la ‘Sina’ kumtumia Mr. Nice kama mpamba video kwa kuelimisha jamii kupitia mistari mizuri iliyopo katika wimbo huo ambao umegusa maisha, marafiki, usaliti, familia, umaskini, starehe, pesa na nk.

Rais wa wasafi, Diamond Platinumz tayari ameweka wazi kuhusu uwezekano wa kumsaidia Mr.Nice ili kurejesha makali aliyokuwa nayo miaka ya nyuma na kumfanya awe jeuri ya matumizi makubwa ya pesa.

Na kuhusika kwenye video ya Harmonize na maudhui ya wimbo huo ni maandalizi ambayo Diamond Platinumz ameyapanga kwa Mr.Nice kumuandaa na ujio wake mpya.

Aidha Mr.Nice alipata nafasi ya kuzungumza na amesema katika maisha yake amekutana na mikasa mingi sana lakini ilikua nafasi ya kujifunza maisha ya kila namna na hivyo hajutii chochote katika yale aliyoyapitia.

”Hata ufanye nini, mimi ni huyu huyu hakuna kitu kitachobadilika. Hakuna ninachoweza jutia” amesema Mr. Nice.

 

 

Korea Kaskazini yaionya Marekani, yaapa kulipiza kisasi
Hamad : Maalim Seif amepoteza uwezo kukiongoza chama chake