Mwanamuziki Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa yupo mbioni kununua ndege yake binafsi ‘Private Jet’ mwaka huu 2022.

Nyota huyo amedokeza suala hilo wakati akimtakia heri ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa meneja wake Sallam Sk kupitia chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Diamomd amekumbushia mipango waliyokuwa nayo na uongozi wake hadi kufikia hatua ya kufanikiwa kununua gari aina ya Rolls Royce Black Bedge mwaka jana, ambayo ni moja ya magari ya ndoto zake.

Amedokeza kuwa mwaka huu lazima atamiliki ndege yake binafsi ‘Private Jet’ kama sehemu ya kutekeleza moja ya ndoto zake.

“Mwaka 2021 tulinunua Royce Black Bedge kilometa sifuri na mwaka huu tunanunua ndege binafsi, hii ndio maana ya kuwa na uongozi bora” ameandika Diamond.

Akihitimisha kwa kumtakia heri ya kumbukizi ya kuzaliwa meneja wake Sallam Sk.

Mpaka sasa nyota huyo yuko chini ya uongozi wa mameneja watatu ambao ni Babu Tale, Sallam SK pamoja na Mkubwa Fella, ambapo Babu Tale yeye yuko katika upande wa shughuli za muziki za msanii huyo kwa ukanda wa Afrika.

Mkubwa Fella akisimamia masuala kadhaa ya nyota huyo kwa upande wa Tanzania pamoja na Sallam Sk ambaye yeye ni meneja anayeshughulikia kila kinachomuhusu msanii huyo kimataifa.

Diamond platnumz ambaye jina lake halisi ni Nasib Abdul ni miongoni mwa wasanii wakubwa wanaoiwakilisha vyema Tanzania na rekodi zake kadhaa zilizofanikiwa kuvuka mipaka kiasi cha kujizolea maelfu ya wafuasi.

⁣Mafanikio yake yamekuwa wazi kutokana na namna ambavyo ameamua kuyaonyesha kupitia kila hatua ya mipango na masuala kadhaa ambayo amekuwa akiyafanya dhahiri bila kificho.

Pamoja na kumiliki Record Label inayowahodhi wasanii wenye kufanya vizuri kiwamo Zuchu, Rayvanny, Mbosso na Lava lava, Pia ni mmiliki wa kituo cha matangazo Wasafi Media (Wasafi TV and Radio), Zoom Xtra, Cheka Tu pamoja na kampuni ya kubashiri Wasafi Bet.⁣

Nyota huyo kwa sasa yuko kwenye orodha ya wasanii kadhaa Afrika mashariki na pengine Afrika wanaomiliki vitu mbali mbali vya thamani ya juu ikiwamo Magari nk, huku akiwa mbioni kununua ndege yake binafsi.

Ifuatayo ni orodha ya magari ya thamani yenye kumilikiwa na msanii Diamond platnumz.

1: The 2021 Rolls-Royce Cullinan⁣, 2: The Cadillac 3: Escalade Black Edition⁣, 4: The Cadillac Escalade Sky Captain Edition⁣, 5: Toyota Landcruiser V8⁣
6: BMW X6⁣ , 7: QqQToyota Landcruiser TX⁣, 8: Toyota Landcruiser V8⁣

Rais Samia afanya uteuzi
MOI yapewa siku 14 kutengeneza mashine za MRI na CT-SCAN