Njaa ya mafanikio kwa vitendo ya Diamond inayochagizwa na menejimenti yake inayojiita ‘wasaka tobo’ imeendelea kuwinda na hatimaye sasa wanataka kuitoboa Marekani na kupiga kazi na Boss wa Good Music, Kanye West.

Diamond na Kanye West walikutana hivi karibuni kwa habati katika uwanja wa ndege wa Los Angeles baada ya Kanye kuvutiwa na viatu vya mkali wa Ngololo na kumuomba kuvipiga picha.

Akizungumza hivi karibuni katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times Fm, Meneja wa Diamond Platinumz, Babu Tale alisema kuwa baada ya wawili hao kukutana katika uwanja huo wa ndege, kwa dakika chache Diamond alijitambulisha haraka na kuelezea kazi zake ili kumvuta rapa huyo nguli duniani na mwisho likatengenezwa daraja kati ya Menejimenti za wawili hao.

“Tunaendelea kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Kanye West kuhusu kazi, tuendelee kusubiri,” Babu Tale alimwambia mtangazaji wa The Playlist, Lil Ommy.

Huenda Diamond akafuata nyayo za D’Banj na kujikuta kwenye ngoma moja na Kanye West kama ilivyokuwa kwa mwimbaji nguli wa Nigeria, D’Banj aliyesainiwa kwenye label ya Good Music inayomilikiwa naye.

Phil Thompson Ainyima Ushindi Liverpool Kama Itamtumia Sakho
Jose Mourinho Kumjibu Anaeziba Rizki Yake Man Utd