Nyota ya Diamond Platnumz inazidi kung’aa na kumulika hadi nje ya bara la Afrika ambakopia imeanza kukubalika.

Siku chache baada ya kushinda tuzo za AFRIMMA, 2015 na Best African Act (MTV 2015), msanii huyo mzawa wa Tandale, Dar es Salaam sasa atashindana na magwiji wa burudani wanaowakilisha kanda mbalimbali duniani akiwemo mrembo wa dunia wa mwaka 2000, kutoka India, Pyanka Chopra akiwa mshindi wa tuzo ya Best Indian Act.

diamondd

Diamond na Pryanka Chopra watashindania kipengele cha Worldwide Act EMA katika tuzo hizo zinazoandaliwa na MTV!

Priyanka Chopra ni mwanamuziki mrembo mwenye umaarufu mkubwa duniani ambaye tangu ashike taji la mrembo wa dunia aliacha alama ambazo hazifutiki kwenye historia ya mashindano hayo.

Pia, amefanikiwa kuzing’arisha filamu nyingi na kubwa za kihindi na hivi sasa anashiriki katika tamthilia maarufu ya Marekani ya Quantico inayooneshwa na kituo cha ABC.

Diamond na Priyanka watashindana na washiriki wengine kutoka Australia, New Zealand, Ulaya, Latin America na Marekani Kusini.

 

 

 

 

Lowassa Amemkwepa Magufuli..?
Mwalimu Aliyetekwa Na Al Shabaab Aokolewa