Mara baada ya kufanya kolabo na wasanii mbalimbali wenye majina makubwa duniani, msanii wa muziki wa Bongo fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ametangaza ujio wa wimbo wake mpya anaotarajia kuufanya na msanii wa rap toka Marekani, Lil Wayne.

Kupitia mitandao ya kijamii Diamond amewaonesha mashabiki wake kionjo cha wimbo huo ambao amemshirikisha Lil Wayne ingawa hajatoa maelezo ya zaidi kuhusu Kolabo hiyo.

Siku za nyuma kulikuwa na tetesi kuwa Diamond anakuja kufanya Kolabo na wasanii wakubwa duniani baada ya kwenda kukaa Marekani kwa muda wa mwezi mzima.

Hata meneja wake Sallam Sk wakati anafanyiwa mahojiano na kituo cha habari cha Times Fm alifunguka na kusema kuwa kuna kitu kizuri kinakuja baada ya kuulizwa swali juu ya kolabo ya msanii wake ambaye ni Diamond na msanii wa nje na kusema kuwa kuna kolabo inakuja akiwa amefanya na Lil Wayne.

Aidha, Diamond tayari amefanya kolabo na Ne-yo ndani ya Mary you, Rick Ross ndani ya Waka waka, Group la Morgan ndani ya Halleluyah, Omario ndani ya African Beauty na wasanii wengine wakubwa toka Afrika kama Davido, Mr. Flavour na Tiwa Savage.

DC Chongolo azindua zoezi la uandikishaji wa vitambulisho
Chadema kutafakari kumpa Maalim Seif kuwania Urais

Comments

comments