Diamond Platinumz amefunguka na kuwaomba mashabiki wake wasilete utimu kwenye suala la familia yake hasa watoto wake watatu ambao amezaa na wanawake wawili tofauti, Zarina Hassan na Hamisa Mobetto.

Amezungumza hayo kufuatia maneno ambayo yamekuwa yakisambazwa katika mitandao ya kijamii yakidai kuwa Diamond hana upendo na mtoto wake wa mwisho Dylan ambaye amezaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Hivyo ameamua kufunguka na kusema hawezi kumtenga wala kumbagua mtoto wake yeyote kwani wote ni watoto wake na anawapenda sana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond Platinumz ameandika hivi.

”This is my Kid and will  forever be my kid, tena my beloved kid…Hakuweza kuwepo kwenye clip iliyopita sababu @lukamboofficial hakuwa na clip ya mimi na yeye ya hivi karibuni  na si vinginevyo. Halafu cha kuongeza, msiniletee uteam wenu kwa watoto zangu! they are all my kids, Nawapenda na siwezi mtenga wala kumbagua yeyote” ameandika Diamond.

Kwenye swala la watoto Diamond Platinumz yupo makini sana kwani hivi karibuni tumeona mama mzazi wa Dylan, mwanamitindo, Hamisa Mobetto amefunguka juu ya nyumba ya ghorofa aliyonunuliwa yeye na mwanae maeneo ya Mbezi Bahari Beach.

Aidha tutaendelea kujua mengi juu ya maisha ya staa huyu wa maziki kufuatia kipindi chake ambacho kimeanzishwa kinachojulikana kama ”The Realty Life of Wasafi” kinachoruka katika chaneli ya Wasafi Tv.

Ajali ya Noah yaua watano Mtwara
Hii ndio sababu ya Ndugai kumtimua mbunge wa CUF bungeni

Comments

comments