‘Katika’ ni wimbo mpya wa Navy Kenzo (Nareel na Aika) wakiwa wamemshirikisha Diamond Platnumz kutoka Wasafi.

Kama kawaida katika mashairi ya Diamond lazima ukutane na majina ya watu wake wa karibu sana katika maisha yake kama vile mama yake, wapenzi wake waliopita, watoto wake, wasanii wake, wachezaji wake muda mwingine hadi mameneja wake.

Katika wimbo wa ”Katika” ambao ameshirikishwa amewataja wapenzi wake wa zamani ambapo amesikika akimtaja Wema Sepetu akimsifia juu ya umbo lake la kuvutia.

Lakini pia katika mashairi ya Daimond ameleta uchokozi kwa kumtaja Hamisa Mobetto juu ya skendo yake iliyovuma siku chache zilizopita zikimuhusiha mrembo huyo na mambo ya kuroga.

Katika wimbo huo (dakika ya 2:52) Diamond ameimba hivi ”Tunguri zimenibamba na Mobetto”.

Aidha, mtindo huo wa kuimba kwa kutaja majina ya watu maarufu hapa nchini umekuwa mtindo unaotumiwa na wasanii wengi hapa nchini.

Taazama hapa chini.

Madaktari walipishwa bilioni 70 kwa uzembe wa kumtahiri mtoto wa siku 18
Fastjet Tz yapiga moyo konde msaada wa kifedha kusitishwa

Comments

comments