Mwanadada kutoka nchini Ethiopia Genzebe Dibaba, amefanikiwa kuwatoa nishai wapinzani wake katika mbio za mita 1500 kwenye michuano ya riadha ya dunia inayoendelea nchini China katika mji wa Beijing.

Dibaba alitumia muda wa dakika  4 Sekunde 08 na alama 09 kufikia lengo la ushindi katika mbio hizo na alifanikiwa kuvishwa mdali ya dhahabu.

Dibaba, alimashinda mpinzani wake wa karibu kutoka nchini Kenya  Faith Kipyegon, ambaye alitumia muda wa dakika 4 sekundu 8 na alama 96 akifuatiwa na Sifan Hassan kutoka nchini Uholanzi aliyetumia muda wa dakika 4 sekunde 9 na alama 34 huku mshiriki kutoka Uingereza Laura Muir akimaliza kwenye nafasi ya tano.

Mwadada huyo mwenye umri wa miaka 24, Bado anaendelea kushikilia rekodi ya dunia aliyoiweka mwaka 2012, katika michuano ya duniani ambayo ilishuhudia washiriki wakikimbia katika uwnaja wa ndani.

Wakenya Wabainika Kutumia Dawa Za Kuongeza Nguvu
Mrembo Wa Miaka 16 Akiri Kuwa Gaidi, Amiliki Mabomu