Wakati ikiaminika kuwa kipa Deogratius Muishi ‘Dida’ yupo njiani kwenda nje kucheza soka la kulipwa huku wengine wakisema anaweza kuelekea Singida United, kipa huyo amerejea kwa mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans.

Dida ambaye hakuwa katika mazoezi ya pamoja na wenzake, jana alikuwa mmoja wa wachezaji waliofanya mazoezi kwenye mazoezi ya Gym akiwa na mastaa wengine wa Young Africans  na hivyo kufanya tetesi za kuwa anataka kuondoka hapo kuwa katika kizungumkuti.

Dida hakutaka kuzungumzia zaidi juu ya usajili wake lakini bado haijafahamika kama ndiyo karejea moja kwa moja au la, kwa kuwa hata baadhi ya watu wa ndani wa Yanga walishanukuliwa wakisema kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Simba na Azam FC yupo njiani kuondoka.

IGP Sirro aanza kulisuka upya Jeshi la Polisi
Madam Flora amnyoshea kidole aliyemzushia uongo