Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ametaja kikosi cha wachezaji 23, ambacho kitashiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016) zitakazofanyika kuanzia mwezi ujao.

Deschamps amemuita mshambuliaji wa Arsenal,  Olivier Giroud, huku akimuweka katika kikosi cha kusubiri mshambuliaji Hatem Ben Arfa ambaye ameonekana kuwa na msimu mzuri akiwa na klabu ya Nice inayoshiriki ligi ya nchini Ufaransa.

Wengine waliotajwa kwenye kikosi hicho ambacho kitakuwa na jukumu la kuwa mwenyeji wa fainali za Euro 2016, ni kiungo wa klabu bingwa nchini England, Leicester City, N’Golo Kante pamoja na kiungo mshambuliaji wa West Ham Dimitri Payet.

Hata hivyo kocha Deschamps, anatarajiwa kutaja kikosi cha mwisho atakachoingia nacho mashindanoni Mei 31, ambapo itakua tarehe ya mwisho ya kuwasilisha majina ya wachezaji wa timu shiriki mbele ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.

Kikosi kamili kilichotajwa na kocha Deschamps upande wa makipa yupo Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Olympique Marseille) na Benoit Costil (Stade Rennes)

Mabeki: Raphael Varane (Real Madrid), Laurent Koscielny (Arsenal), Eliaquim Mangala (Manchester City), Jeremy Mathieu (Barcelona), Patrice Evra (Juventus), Bacary Sagna (Manchester City), Lucas Digne(AS Roma) na Christophe Jallet (Olympique Lyon)

Viungo: Paul Pogba (Juventus), Blaise Matuidi (Paris St Germain), Lassana Diarra (Olympique Marseille), N’Golo Kante (Leicester City), Yohan Cabaye (Crystal Palace) na Moussa Sissoko (Newcastle United)

Washambuliaji: Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Dimitri Payet (West Ham United), Anthony Martial(Manchester United), Kingsley Coman (Bayern Munich), Olivier Giroud (Arsenal) na Andre-Pierre Gignac(UANL Tigres)

Kikosi cha akiba: Alphonse Areola (Villarreal), Hatem Ben Arfa (Nice), Kevin Gameiro (Sevilla), Alexandre Lacazette (Olympique Lyon), Adrien Rabiot (Paris St Germain, Morgan Schneiderlin (Manchester United), Djibril Sidibe (Lille) na Samuel Umtiti (Olympique Lyon).

Viongozi Wa Arsenal Wamfikiria Upya Arsene Wenger
Ibrahim Ajib Aanza Vyema Afrika Kusini

Comments

comments