Kocha wa mabingwa wa soka duniani (Ufaransa) Didier Deschamps, ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kitakachoanza kampeni ya kusaka ubingwa wa barani ulaya (UEFA Nations League) mapema mwezi Septemba.

Mabingwa hao wa dunia watanza kampeni ya kusaka taji la Ulaya kwa kupambana na Ujerumani Septemba 06, na siku tatu baadae watapambana na Uholanzi.

Kocha Deschamps hajafanya mabadiliko yoyote kwenye kikosi chake, zaidi ya kumuacha mlinda mlango wa klabu ya Olympique de Marseille Steve Mandanda Mpidi, ambaye nafasi yake imechukuliwa na Benoit Costil wa Bordeaux.

Mandanda ameachwa kwenye kikosi hicho kufuatia majeraha nyama za paja aliyoyapata wakati wa mchezo wa ligi ya Ufaransa, ambapo timu yake ilipoteza kwa kufungwa bao moja dhidi ya Nimes mnamo Agosti 19.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 33, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma manne.

Kikosi kamili kilichoitwa na kocha Deschamps upande wa makipa yupo Alphonse Areola [Paris Saint-Germain], Benoit Costil [Bordeaux] na Hugo Lloris [Tottenham Hotspur].

Mabeki: Lucas Hernandez [Atletico Madrid], Benjamin Pavard [Stuttgart], Samuel Umtiti [Barcelona], Presnel Kimpembe [Paris Saint-Germain], Adil Rami [Marseille], Raphael Varane [Real Madrid], Benjamin Mendy [Manchester City] na Djibril Sidibe [Monaco].

Viungo: N’Golo Kanté [Chelsea], Paul Pogba [Manchester United], Blaise Matuidi [Juventus], Corentin Tolisso [Lyon] na Steven Nzonzi [Roma].

Washambuliaji: Moussa Dembélé [Barcelona], Antoine Griezmann [Atletico Madrid], Florian Thauvin [Marseille], Nabil Fakir [Lyon], Olivier Giroud [Chelsea] na Kylian Mbappé [Paris Saint-Germain].

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 31, 2018
Luka Modric mchezaji bora Ulaya

Comments

comments