Aliyekuwa Mchezaji wa Yanga Princess Didier Fetty kupitia ukurasa wake wa Instagram amewaaga Wananchi, huku akieleza kuwa ‘Jambo moja ndio mwanzo wa Jambo lingine’.

Nyota huyo mwenye makombe mawili ya Ligi Kuu ya Wanawake mpaka Sasa, amehudumu Yanga Princess katika nafasi tofauti Dimbani kama vile 2, 3, 6 na hata Kiungo Mshambuliaji.

Fatuma amesema anaushukuru uongozi wa Yanga Princess kwa kumpa ushirikiano kwa kipindi chote lakini kama Mchezaji atarejea tena dimbani hivyo Mashabiki wake wasiwe na presha.

“Nawashukuru Wachezaji wenzangu, Benchi la Ufundi pamoja na Viongozi wangu wa Yanga Princess kwa kunipa sapoti Katika kipindi chote ambacho tulikuwa pamoja, nawatakia maandalizi mema na mafanikio msimu ujao” amesema Fatuma.

Ameongeza kuwa, licha ya kwamba bado ajapata ofa yoyote mpaka Sasa, lakini anaamini mambo mazuri yanakuja hivyo Kila kitu kitakuwa sawa.

“Timu yoyote nafanya nayo Kazi, iwe ndani au nje ya Nchi, muhimu ni kufikiana makubaliano tu, nahitaji kucheza zaidi, mpira bado unanidai, sijakata tamaa baada ya kuondoka Yanga, maisha yataendelea hata iwaje” amemaliza hivyo ‘DIDIER’

Bei ya umeme miradi midogo shilingi 1600
Simba SC yajibu FUMBO la Nembo ya Mdhamini