Mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Diego Costa ameuomba uongozi wa klabu ya Chelsea, kumrejesha nchini kwao ili akaitumie tena klabu ya Atletico Madrid.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star la nchini England, mshambuliaji huyo amewasilisha ombi hilo kwa uongozi wa The Blues, kwa kutaka auzwe ili aweze kurejea mikononi mwa Diego Simione.

Hata hivyo sababu za Costa kutaka auzwe na kurejeshwa mjini Madrid hazijaelezwa wazi, japo kuna tetesi zinadai kwamba hapendezwi na maisha ya nchini England sambamba na kuchoshwa na mihangaiko ya hapa na pale anayoipata katika ligi ya nchini humo.

Sehemu ya mihangaiko anayoipata katika ligi ya nchini humo, ni kukamiwa sana na baadhi ya wachezaji wa klabu pinzani, hatua mbayo humsababishia kufungiwa na FA, mara kwa mara kutokana na kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu pale anapochokozwa.

Gazeti la Daily Star limeendelea kuripoti kwamba, endapo ombi la Diego Costa litakubaliwa huenda akauzwa kwa kiasi cha Pauni milioni 40, kufuatia baadhi ya vipengele vilivyopo katika mkataba wake huko magharibi mwa jijini London.

Chelsea wameripotiwa kukaribia kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Michy Batshuayi, baada ya kukubali kutoa ada yake ya uhamisho ya Pauni milioni 33, akitokea Olympic Marseille.

Hata hivyo kama itatokea Costa anaondoka, Chelsea itawalazimu kumsaka mshambuliaji mwingine ambaye atakabidhiwa jukumu la mspaniola huyo.

Ukubwa wa ''My life Remix'' ni Tofauti na Nilivyoifikiria -Dogo Janja
Video: Tundu Lissu amepata dhamana, haya hapa aliyoyaongea