Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan Diego Milito, amesema ipo haja kwa viongozi wa klabu hiyo kumtangaza Leonardo Nascimento de Araújo kama mkuu wa benchi la ufundi, baada ya kuondoka kwa Frank de Boer mwanzoni mwa juma lililopita.

Milito ambaye kwa sasa amestaafu soka, amesema Leonardo anastahili kuchukua nafasi hiyo kutokana na uzoefu mkubwa alionao katika ligi ya nchini Italia (Serie A).

Amesema anaamini kinachoisumbua Inter Milan mpaka kufikia hatua ya kupoteza muelekeo tangu alipoondoka Roberto Mancini miezi mitatu iliyopita, ni kushindwa kuwa na mkuu wa benchi la ufundi mwenye uzoefu na ligi ya Serie A.

“Ninamfahamu Leonardo, ana viwnago vya hali ya juu vya ufundishaji soka, pia ana uzoefu wa kutosha katika ligi ya nchini Italia, Viongozi wa Inter Milan wanapaswa kumtazama mtu huyu,” alisema Milito.

Leonardo aliwahi kukinoa kikosi cha Inter Milan msimu wa 2010–2011 na kabla ya hapo alikuwa meneja wa AC Milan msimu wa 2009–2010.

TFF: Young Africans Vs Ruvu Shooting Kupigwa Kesho
Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi Shinyanga kufuatia vifo vya watu 18