Baada ya kuthibitika mlinda mlango kutoka nchini Brazil Alisson Ramses Becker ataihama AS Roma na kujiunga na Liverpool kwa ada ya Euro milioni 75 ambazo ni sawa na Pauni milioni 66.9, mshambuliaji Diego Perotti amemtakia kila la kheri na kusema hawatotetereka kwa kuondoka kwake.

Peroti amesema kuondoka kwa Alison ni hatua kubwa kwa klabu na kwake binafsi, lakini anaamini uongozi wa AS Roma utaweza kuliziba pengo la mlinda mlango huyo, kama walivyofanya wakati alipondoka mshambuliaji kutoka nchini Misri Mohamed Salah.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Argentina, amesema AS Roma miaka yote imekua na desturi ya kuwainua wachezaji, na wanapoonekana na klabu nyingine huendelea na utaratibu wa kuwanyanyua wengine.

“Alisson ni mchezaji mwenye kufahamu wajibu wake anapokua langoni, kuondoka kwake ni jambo zuri kwa klabu na kwake binafsi, lakini ninakuhakikishia As Roma itakua na mlinda malango mahiri zaidi, kwa msimu ujao wa ligi,” alisema Perotti alipohojiwa Sky Sport Italia.

“Uongozi umekua na taratibu nzuri wa kuwainua wachezaji kila mwaka, ninaamini wataifanya kazi ya kumleta mlinda mlango meingine ambaye ataweza kuitetea klabu, katika kipindi chote atakachokaa klabuni hapa.”

Alisson anatarajiwa kuelekea mjini Liveropol leo Alkhamis kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya, baada ya kuafikiana na uongozi wa klabu ya Liverpool maslahi binafsi.

Taarifa zinaeleza kuwa, mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano.

Alisson anaondoka AS Roma huku akiacha kumbukumbui ya kucheza michezo 37 msimu wa 2017/18 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 28.

Video: Haijapata kutokea, Tundu Lissu amvaa JPM
Gianfranco Zola kumsaidia Maurizio Sarri Stamford Bridge

Comments

comments