Klabu ya Atletico Madrid inatajwa kuwa kwenye mpango wa kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic itakapofika Januari 2018 (Dirisha Dogo), pindi adhabu yao iliyotolewa na FIFA ya kutosajili itakapofikia kikomo.

Ibrahimovic amekua akiwindwa na meneja wa Ateltico Madrid Diego Simeone, ambaye anaamini uwezo wa mshambuliaji huyo unaweza kubadili mfumo anaoutumia kwa sasa kikosini kwake.

Mara kadhaa Simeone aliripotiwa kumfuatilia Ibrahimovic ambaye aliwahi kuitumikia FC Barcelona, na anaamini hadi itakapofika Januari 2018 atakua amepona jeraha la mguu, ambalo alilipata wakati wa mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht mwezi April mwaka huu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, anatarajiwa kuwa mchezaji huru kuanzia Julai mosi mwaka huu, baada ya mkataba wake na Man Utd kufikia kikomo

Taarifa za Atletico Madrid kumuwania Ibrahimovic, zinafuta tetesi za mshambuliaji huyo kuwa na mpango wa kutimkia nchini Marekani, ambapo tayari klabu ya LA Galaxy inatajwa kuwa kwenye harakati za kumsajili.

Malinzi, Mwesigwa wakamatwa, watuhumiwa kutumia vibaya ofisi
Paolo Maldini Atupwa Nje Aspria Tennis Cup