Kocha wa klabu ya Atletico Madrid Diego Pablo Simeone amesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuinoa klabu hiyo inayoshiriki katika ligi kuu ya La Liga nchini Hispania.

Kumekuwa na tetesi za kocha huyo kutaka kuhamia katika klabu ya Inter Milan lakini tetesi hizo zimezimwa rasmi baada ya kocha huyo raia wa Argentina kusaini mkataba mpya.

Simeone mwenye umri wa miaka 47 aliwachezea vigogo wa Italia Inter Milan kuanzia mwaka 1997 hadi 1999 akiichezea timu hiyo jumla ya michezo 57 na kufunga mabao 11.

Atletiko Madrid itazidi kutoa ushindani mkubwa kwa vilabu vya Real Madrid na Barcelona kwani Simeone amesaini mkataba mpya ambao unamfunga Atletico Madrid kwa misimu miwili zaidi mpaka Juni 30 mwaka 2020.

Kocha huyo mwenye mbwembwe nyingi awapo uwanjani anapendwa sana na mashabiki wa Atletico Madrid na    wamejenga imani kubwa kwake kufuatia kushinda taji la La Liga kama mchezaji na baadaye kocha.

 

Mkuu wa Kikosi cha Jeshi Lesotho auawa
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Septemba 6, 2017