Aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya England Sven-Goran Eriksson amesitisha mpango wa kuajiriwa na chama cha soka nchini Iraq (IFA), kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari duniani la Reuters, kocha huyo kutoka nchini Sweden amekataa mpango huo, kutokana na baadhi ya mambo katika mazungumzo na uongozi wa IFA kutokwenda sawa, kabla ya kusaini mkataba wa kuanza kazi.

Eriksson alikua anatarajiwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Iraq, kuelekea katika fainali za mataifa ya bara la Asia zitakazochezwa mwanzoni mwa mwaka 2019, huko Falme za kiarabu.

Timu ya taifa ya Iraq ambayo iliwahi kutwaa ubingwa wa fainali hizo mwaka 2007, imepangwa kundi moja na Iran, Vietnam na Yemen, katika fainali hizo ambazo zitaanza rasmi Januari 05.

Dhumuni kubwa la IFA kumshawishi Erickson kukubali majukumu ya kukinoa kikosi chao, lilikua ni kuiwezesha timu yao kufanya vyema katika fainali za Asia, na baadae kuhakikisha wanafuzu kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 zitakazounguruma nchini Qatar.

Mnangagwa aibuka kidedea uchaguzi mkuu Zimbabwe
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 3, 2018