Taarifa za kiungo na nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure kuwa mbioni kuikacha Man City mwishoni mwa msimu huu, zinaendelea kushika kasi.

Wakala wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, Dimitri Seluk amethibitisha kuanza mazungumzo na baadhi ya klabu za barani Ulaya, ili kuangalia uwezekano wa kumtafutia mchezaji wake mahala pengine pa kusakata soka.

Klabu za Bayern Munich, Juventus pamoja na Paris Saint-Germain zimetajwa kuwa katika mazungumzo na wakala huyo, ambaye mara kwa mara amekua mstari wa mbele kutetea maslahi ya Toure.

Seluk ameamua kufanya hivyo, kutokana na agizo alilowapa viongozi wa Man City la kutoa jibu la kuendelea na Toure ama kumruhusu aondoke mpaka itatakapofika mwishoni mwa sikuku ya pasaka na sasa imeonekana mambo hayajakaa sawa.

“Nilitoa muda kwa viongozi wa Man City ili waweke jibu hadharani la kuendelea na Toure, lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea zaidi ya ukimya uliotawala, hivyo sina budi kuanza mikakati ua kufanya mazungumzo na wengine.” Alisema Seluk.

“City wanashindwa kufanya maamuzi sahihi, na sijajua kwa nini inakua hivyo, lakini wanatakiwa kufahamu kwamba kazi ya Yaya ni kucheza soka na anatakiwa ajue mustakabali wake.” Aliongeza wakala huyo kutoka nchini Urusi

Mzozo uliopo kati ya wakala huyo na viongozi wa Man city ni kusainiwa kwa mkataba mpya wa mchezaji wake kufuatia mkataba wa sasa kusaliwa na muda wa miezi 12, ambao unamuwezesha kulipwa mshahara wa pauni laki mbili na ishiriki (220,000) kwa juma.

Charles Boniface Mkwasa Anadai Mamilioni Ya Shilingi
Mayanja: Isihaka Amebadilika Kitabia