Wakala wa Yaya Toure (Dimitri Seluk) amejibu mapigo kwa kauli ya jazba ya Pep Guardiola juu ya hatima ya mchezaji wake klabuni hapo.

Guardiola aliwaambia waandishi kuelekea mchezo wa Kombe la EFL dhidi ya Swansea City kwamba kwamwe hatamjumuisha Toure kwenye kikosi mpaka atakapoomba radhi kufautia kauli iliyotolewa na Seluk baada ya jina lake kuondolewa kwenye kikosi cha City Ligi ya Mabingwa.

Awali Seluk alisema kwamba Guardiola anapaswa kuomba radhi kwa unyanyasaji anaomfanyia mteja wake, lakini bosi huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich ameonekana kuchuikizwa na kauli hiyo.

“Toure lazima aombe radhi kwa wachezaji wenzake na kwa klabu. Kama hatafanya hivyo basi hatacheza tena,” amesema Guardiola.

Seluk ameonesha kutokubaliana na kauli hiyo ya Guardiola na kusema kwamba ushindi mfululizo wa mechi nane kwa kocha huyo si kigezo cha yeye kujiona mfalme.

“Michezo hii michache ambayo Guardiola ameshinda isimfanye ajione mfalme,” Seluk amesema.

“Naishi Ulaya na naongea chochote ninachojisikia na Guardiola hawezi kunizuia mimi.

“Kwa kipi hasa nimuombe msamaha? sawa, Nitamuomba radhi Guardiola endapo tu ataomba radhi kwa Manuel Pellegrini kwa kitendo alichomfanyia.

“Kama wewe ni mtu muungwana, suala kama hili haliwezi kutokea. Pellegrinin alisaini mkataba mpya mwaka mmoja uliopita halafu baadaye Guardiola anatangazwa kuja kushika mikoba yake. Pellegrini alikuwa ni mtu muungwana sana.”

Taraka ya muigizaji Brad Pitt na Angelina Jolie ni gumzo.
Gundogan: Klopp Alinishauri Kujiunga Man City