Uongozi wa klabu ya Manchester United umeanza kufanya mazungumzo na beki wa pembeni wa mabingwa wa soka nchini Ureno FC Porto, Diogo Dalot.

Taarifa zilizotolewa usiku wa kuamkia leo na kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England zimeeleza kuwa, Man Utd wameanza mazungumzo hayo, kufuatia uhitaji wa beki wa kulia katika kikosi chao kwa msimu ujao wa ligi.

Meneja wa Jose Mourinho amekua akitoa msukumo kwa viongozi wa juu wa klabu hiyo, kuhakikisha wanafanikisha mpango wa kupatikana kwa beki wa kulia, na pendekezo lake la kwanza limemlenga Dalot mwenye umri wa miaka 19.

Mpango wa usajili wa mchezaji anaecheza nafasi ya beki wa kulia, umezuka kufuatia mustakabali wa beki kutoka nchini Italia Matteo Darmian kuwa shakani, hasa baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Tayari uongozi wa FC Porto umeshaweka wazi thamani ya Dalot ambaye anaitumikia timu ya taifa ya Ureno chini ya miaka 21 kwa kusema, beki ataondoka klabuni hapo kwa kiasi cha Euro milioni 20 ambazo ni sawa na Pauni milioni 17.4.

Dalot alianza kucheza katika kikosi cha kwanza cha FC Porto mwezi Februari mwaka huu, na ameonyesha uwazo mkubwa katika michezo yote aliyocheza hadi mwishoni mwa msimu wa 2017/18.

Mahakama yalitupa shauri la kupinga kanuni za maudhui mtandaoni
Watanzania 11 wafutiwa kesi Afrika Kusini