Msemaji wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten amewataka mashabiki wa Klabu hiyo kuacha tabia ya kulalamika na kuwafundisha viongozi wao cha kufanya bali waende uwanjani kuiunga mkono timu yao.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa tabia ya kuwapangia viongozi na kuwafundisha cha kufanya huku wakilaumu si nzuri bali wao kazi yao kubwa ni kwenda uwanjani kuiunga mkono timu yao.

“Tunao mashabiki wengi kwasasa wamekuwa wakizungumza vitu vingi, kusema watu, kutukana watu ni wakati sasa wakuacha kufanya hivyo badala yake wajitokeze uwanjani kutoa nguvu ya 12 kusapoti wachezaji,” amesema Ten

Aidha, amesema kuwa watu wengi walikuwa wanamuuliza kwanini hajaenda na timu Botswana ambapo amesema Yanga ni taasisi kubwa na ina wafanyakazi wengi ambao wanafanya majukumu wakati yeye yupo kwenye shughuli zingine za taasisi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa masuala ya benchi la ufundi kupangiwa kikosi yameshapitwa na wakati, kwasababu benchi lina uwanja wake mpana wa kufanya maamuzi kwenye kikosi ili timu ifanye vizuri hivyo kila mtu afanye majukumu yanayomuhusu.

Azam Media wamalizana na Young Africans
Shonza: Siwezi kujibizana na Diamond