Mtangazaji maarufu wa kipindi cha ‘Ala za Roho’ cha Clouds FM ambaye sasa amejitosa rasmi kwenye uimbaji pia, Diva Thee Bawse amesema yuko mbioni kumnasa Bosi wa lebo ya Konvict Music, Akon.

Diva alifunguka mpango huo katika mahojiano aliyofanya na Lil Ommy kwenye The Playlist ya Times FM hivi karibuni, ikiwa ni sehemy ya mpango wa kuikamilisha albam yake ya ‘Ala za Roho’.

“Sasa hivi nawasiliana na Akon, kama tutaweza kumpata akatusaidia baadhi ya vitu. Nasikia ni mtu ambaye yuko fresh sana. Naangalia jinsi ambavyo tunaweza kumpata ili tuweze kufanya kitu kizuri,” alifunguka.

Diva ambaye alianza na muziki kabla hajawa mtangazaji, amesema kuwa albam yake ijayo itakuwa pia na wasanii wengi wakubwa kutoka Afrika kama Run Town, Brick and Lace, Khaligraph Jones, P-Unit na wengine kutoka ndani ya nchi.

Taarifa kutoka Ikulu kwa JPM muda huu
Video: Viongozi wa dini liombeeni Taifa - Makonda

Comments

comments