Mtangazaji maarufu wa kipindi cha radio kinachofahamika kama Ala za Roho, Diva the Bowse ameanzisha kampeni yake itakayoitwa Dreams, Hopes, Wishes itakayomsaidia kuchangisha kiasi cha pesa dola 7000 kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa unaomsumbua anaotarajiwa kutibiwa nje ya nchi akidai kuwa kwa sasa hana kiasi hiko cha pesa.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameweka wazi tatizo linalomsumbua na kumfanya kwa kipindi kirefu kutokuwa na uwezo wa kupata mtoto.

Diva amesema anasumbuliwa na ugonjwa wa kuziba kwa mirija ya uzazi kitaalamu unajulikana kama Bilateral Cornual Block ambapo madaktari wamesema kwa tatizo hilo kupata mtoto kwa njia ya kawaida si jambo rahisi na matibabu yake hufanyika nje ya nchi.

Hivyo ameomba msaada kwa wasamaria wema dola 7000 sawa na shilingi Milioni 15 za Kitanzania  kwa ajili ya kuzibua mirija hiyo iliyoziba.

Diva amesema ameamua kuweka hadharani tatizo hilo bila aibu wala uoga kwani inawezekana wapo wengi wanaosumbuliwa na tatizo hilo na wanahitaji msaada.

Diva ameomba kwa yeyote yule atakayeguswa na suala lake amchangie kupitia akaunti yake iliyopo katika ukurasa wake wa instagrama na namba za Tigo pesa alizoziweka katika ukurasa huo.

Aidha Diva ameandika ujumbe huo kwa masikitiko makubwa sana kwani amekuwa akitafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio.

Mwanafunzi kidato cha 4 auawa kikatili, 'achunwa ngozi'
Mke wa Mzee Majuto afukuzwa aomba msaada kwa watanzania