Mtangazaji wa Clouds Fm ambaye pia ni msanii wa Bongo Flava, Diva amegeuka mbogo mjeruhiwa baada ya kusoma kipande cha gazeti moja kubwa nchini likimnukuu rapa Billnas akidai kuwa mrembo huyo anajigonga kwake.

Billnas na Linah

Billnas na Linah

Diva ameoenesha kuchukizwa na habari hiyo ambayo ameeleza kuwa ana imani imetokana na matamshi ya Billnas kama alivyonukuliwa na mwandishi wa habari hiyo. Mwimbaji huyo amedai kuwa hiyo ni mbinu chafu ya rapa huyo akishirikiana na mpenzi wake Linah kutafuta ‘kick’ kupitia jina lake, huku akilaani vikali uandishi wa habari wa aina hiyo.

Kutokana na hilo, Diva ambaye amemshirikisha Billnas na Mr Blue kwenye wimbo wake mpya ‘Baby Boy’, ameapa kuondoa sauti ya rapa huyo.

‘Wee mwandishi wa hili gazeti ni Mpumbavu na Billnass Kama Umeongea kweli hii ni Mpumbavu na Natoa Verse yako kwenye wimbo wangu. Vibongo fleva artist vinapenda Kiki asa Billnass nijigonge kwako ili iweje?!,” Diva ameandika Instagram akiambatanisha na maneno yenye ukakasi.

Alisema kuwa anachoamini, Linah ameungana na Billnas kutengeneza uongo huo kutokana na wivu wa mapenzi. Amesema anaamini Linah alikuwa anaona wivu kwakuwa amekuwa akipost picha akiwa na rapa huyo.

Hata hivyo, Billnas ameiambia Clouds Fm kuwa alishtushwa kuona habari hiyo iliyoandikwa kwenye magazeti pamoja na kile alichokiandika Diva. Alisema alitarajia Diva angempigia simu kumuuliza kabla ya kuchukua hatua hiyo.

Kuhusu kuondolewa kwenye wimbo huo, alisema anaona itakuwa vizuri zaidi kwani wimbo huo haumsogezi kokote.

Nash MC afunguka kuhusu hali ya Fanani wa HBC baada ya kumtembelea ‘Rehab’
Ukimya wa washindi watano wa BSS Wamfungua Kinywa Madam Rita