Mtangazaji wa Clouds FM kipindi cha ala za roho, Diva The Bawse amesema kitendo cha Alikiba kumwacha Jokate ni kosa kubwa analoweza  kujutia baadae hivyo amemtaka afanye kitu kurudisha mahusiano yake na Jokate.

Diva The Bawse hajawahi kuwa na mahusiano mazuri na Jokate lakini hiyo si sababu ya yeye kutokuongelea mazuri ya mwanadada Jokate.

Diva amesema Ali amepoteza kitu kizuri sana, kwani Jokate alikuwa ni msichana ambaye muda wote alikua tayari kumsaidia Ali kwa jambo lolote hasa katika shughuli zake za kimuziki.

“Ali amepoteza a very good thing,” amesema Diva. “She was there to support him, do you remember when everyone was against Ali? Kwahiyo amepoteza a very good thing ambaye angemsaidia vitu vingi in a way of yeye as mwanamuziki wa kiumbe ambaye girls love him, mtu mwenye uwezo wa kumweka sehemu sahihi. Kwahiyo amepoteza kitu kizuri sana Ali, inabidi afanye kitu arudi pale,” amesisitiza Diva.

“You can see, she was proud, anamsifia anampost, unajua alikuwa ametake risk kiasi gani? Someone is not your husband, and you are there to support him like that and then unasikia wamebreak-up, like what’s wrong with Ali?”

Diva anasema kuwa alidhani kuwa Alikiba angekuja kumuoa Jokate.

Instagram yampa Ben Pol ‘kolabo’ na Ray J wa Marekani
Maombi ya 'kumtoa' Lissu yaanza mchakato Mahakama Kuu