Wananchi wa Kata ya Inyeze wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamelalamika kwa diwani wa kata hiyo kwa kuvamiwa na kundi kubwa la fisi kijijini hapo.

Hayo yamesemwa katika kikao cha Baraza la Madiwani na Diwani wa Kata hiyo, Lucas Makulumo ambapo amesema kuwa Fisi hao wanaonekana muda wote wa mchana na usiku.

Makulumo amemtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Abel Shija, aeleze halmashauri ina mpango gani juu ya wanyama hao waliovamia Kata yake na kuhatarisha maisha ya wananchi wake.

Aidha Diwani huyo amelieleza baraza hilo kuwa matukio ya wanyama hao kuvamia maeneo ya kata yake yamekuwa ya kawaida, hali inayowatia hofu wananchi wake, wakiwamo watoto wanakwenda shule.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo amewataka wataalamu wa Maliasili na Wanyamapori kuhakikisha wanyama hao wanaondolewa kabla hawajaleta madhara kwa wananchi.

Raila aapishwa kama Rais wa watu, wengi wahoji
Wafahamu viongozi wa Afrika waliowahi kujiapisha