Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani mstakihi meya wa  halmashauri ya manispaa ya Iringa, Alex Kimbe kupitia chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) kwa makosa mawili ya jinai ya kuomba na kupokea rushwa .

Akizungumza leo na vyombo vya habari ofisibni kwake, Kaimu kamanda wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Mweli Kilimali  amesema kuwa meya huyo alipokea kiasi cha shilingi milioni 2 kutoka kwa mteja wao .

Amesema kuwa tukio la kukamatwa meya huyo lilitokea Novemba 15 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika Hotel ya Gentle Hills mjini Iringa .

Aidha, amesema kuwa Meya Kimbe alipokea fedha hizo za mtego wa rushwa akiwa kwenye gari yake aina ya nadia yenye rangi ya Marron ikiwa na namba za usajili T 456 CKD iliyokuwa imeegeshwa katika eneo la kuegesha magari kwenye hoteli hiyo.

“Maafisa wa Takukuru waliweza kumfuatilia Meya huyo kwa muda mrefu na hivyo kuweza kumkamata akiwa  amekwisha pokea fedha hizo za mtego kutoka kwa mtoa taarifa wetu,“amesema Kilimali

Hata hivyo, Meya huyo anatuhumiwa kwa kosa la kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 na baada ya mtoa taarifa kujitetea hatokuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo mtuhumiwa alikubali kupokea shilingi milioni 2.

 

Mbunge CUF asababisha mbunge wa Chadema kufukuzwa
Magunia 17 ya Bangi yakamatwa mkoani Pwani

Comments

comments